Posts

Watu waliotoweka mwaka 1942 wapatikana kwenye barafu Uswisi

Image
Brafu inayoyeyuka nchini Uswisi imefichua miili miwili inayoaminiwa kuwa ya mtu na mkewe waliotoweka miaka 75 iliyopita. Marcelin na Francine Dumoulin walitoweka wakati walienda kuchunga ng'ombe wao katika milima ya Alps mwaka 1942. Watu hao walikuwa na watoto saba. Mtoto wao wa mwisho wa kike ambaye sasa ana umri wa 79, anasema habri hizo zimemletea utulivu na anataka kuwafanyia maziko mema. "Tulitumia maisha yetu yote kuwatafuta," alisema Marceline Udry-Dumoulin. Uchunguzi wa DNA unatarajiwa kufanywa. Polisi wanasema kuwa miili hiyo iligunduliwa wiki iliyopita katika eneo la Tsanfleuron na mfanyakazi kutoka kampuni ya kuteleza kwa barafu ya Glacier 3000.

Kisiwa chashinda shindano la ukweaji mnazi

Image
Kisiwa cha Cook ndio bingwa duniani wa shindano la ukweaji minazi ,imeripotiwa. George Iona aliibuka mshindi katika shindano lillilokuwa na wawaniaji 16 ,akishinda kwa uchache kulingana na idhaa ya redio ya Tahiti. Aliupanda mti huo wenye urefu wa mita nane kwa sekunde 5.62 katika shindano hilo lililofanyika katika eneo la kumbukumbu la Tahiti. Alikuwa mbele ya Fiapai Ellio wa Samoa ya Marekani mtu aliyepigiwa upato kushinda. Lengo la shindano hilo jipya ,ni kupanda mti huo haraka iwezekanavyo huku kila mpandaji akipewa fursa mbili za kuweka muda bora zaidi. Hatua hiyo inashirikisha kuvaa kamba katika visigino vya miguu ili kusaidia kukwea kwa garaka. Akizungumza na idhaa ya redio ya Tahiti 1, mwaandalizi Enoch Laughlin amesema kuwa ushindi mkubwa wa bwana Iona uliwashangaza watu wengi, kwa kuwa kila mtu alitarajia kwamba mwanariadha wa Samoa ataibuka mshindi kufuatia ushindi wao katika mashindano ya awali. Mshindi huyo aliwaambia maripota kwamba ni fahari kubwa na furaha...

R Kelly atuhumiwa kwa ''kuwanyanyasa kingono wanawake''

Image
Mwanamuziki wa mtindo wa R&B R Kelly amekana madai kwamba anawazuia wanawake kadhaa katika dhehebu lake analotumia kuwanyanyasa. Wakili wa mwanamuziki huyo alisema kuwa atatumia kila njia kuhakikisha kuwa wale wanaomtuhumu anawakabili kisheria ili kusafisha jina lake. Ripoti ya BUzzFeed imemtuhumu mwanamuziki huyo kwa kuwabadili kimawazo wanawake walio karibu naye kwa lengo la kuimarisha usanii wao wa muziki. Kelly tayari amewahi kukabiliwa na tuhuma za dhulma za kingono lakini hakupatikana na hatia. Amekana kufanya makosa yoyote. Ripoti hiyo iliowanukuu wazazi watatu inasema kuwa hawajawasiliana na wanao kwa miezi kadhaa ,na kwamba wanawake hao wote wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 18 walikuwa wakidhibitiwa na msanii huyo. Udhibiti huo unashirikisha chakula wanachokula na nguo wanazovaa ,wakati gani wa kuoga na kulala mbali na kufanya tendo la ngono yote hayo yakirekodiwa na msanii huyo. Wanachama watatu walio karibu na mwanamuziki huyo pia walihojiwa na kusema kuwa ...

Usher Raymond azuru mbuga ya Serengeti Tanzania

Image
Msanii wa Marekani Usher Raymond yuko ziarani nchini Tanzania akitembelea eneo la uhifadhi wa wanyama pori la Serengti National Park. Bwana Raymond alichapisha baadhi ya picha akiwa na familia yake katika akaunti yake ya Twitter. Alielezea hali ilivyo katika eneo hilo kama ya kufurahisha . Ripoti za Usher Raymond kuzuru Tanzania zilisambaa kwa haraka nchini humo. Watu wengine maarufu akiwemo mchezaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid David Becham, aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho, mchezaji wa Everton Morgan Schneiderlin ni miongoni mwa wale waliozuri katika sehemu mbali mbali za kitalii nchini humo mwaka huu. Vivutio vya kitalii nchini Tanzania kama vile mbunga ya uhifadhi wa wanyama pori ya Serengeti na mlima Kilimanjaro ni vivutio vinavyoongoza kwa utalii ambapo watu wengi maarufu wametembela.

Mamia waogelea wakiwa utupu Finland kuvunja rekodi

Image
Mamia ya waogeleaji waliokuwa utupu walijumuika kwa pamoja kuogelea katika mto wenye maji baridi katika jaribio la kuvunja rekodi nchini Finland. Washiriki walikuwa wanataka kuvunja rekodi ya dunia ya watu wengi zaidi kuwahi kuogelea kwa pamoja wakiwa utupu. Watu 789 waliokuwa pia wanahudhuria tamasha ya muziki mashariki mwa Finland walijitosa kwenye maji kuogelea wakiwa utupu, waandalizi wanasema. Walifanikiwa kuvunja rekodi ya awali iliyokuwa imewekwa na waogeleaji nchini Australia, kwa kuzidi watu hao kwa watu watatu, taarifa zinasema. Waandalizi wamesema sasa wanasubiri rekodi yao ithibitishwe na maafisa wa Guinness World Records. Hii ni mara ya tatu kwa jaribio la kuvunja rekodi hiyo kuandaliwa nchini Finland, mtandao wa habari wa Yle umesema. Majaribio ya awali mjini Helsinki mwaka 2015 na mwaka 2016 yalivutia watu takriban 300. Waandalizi wa tamasha hiyo ya muziki ya Ilosaari Rock mjini Joensuu walikuwa wamekusubia kuwapata watu 1,000. Sawa na ilivyokuwa katika m...

Juhudi za kuubadilisha mswada wa Obamacare zakwama

Image
Maseneta wengine wawili wa chama cha Republican wanasema kuwa wanapinga mpango wa chama chao, wa kuubadilisha muswada wa afya wa Obamacare hatua iliowawacha viongozi wa Republican na uchache wa kura kufanya mabadiliko hayo. Mike Lee na Jerry Moran wote walitangaza kwamba hawawezi kuunga mkono muswada huo kama ulivyo. Viongozi wa Republican wanashikilia viti 52 katika bunge hilo lenye wanachama 100, na huku wanachama wawili wa Republican wakiupinga muswada huo hawangeweza kuruhusu viongozi wengine kuupinga. Rais Trump aliahidi kuubadilisha muswada wa afya wa rais Obama kama ahadi yake wakati wa kampeni Maseneta hao wawili walitangaza hatua yao mara moja. Huku wakisema kuwa kulikuwa na matatizo mbalimbali kuhusu muswada wa Obamacare, waliongezea kuwa ''hawawezi kuidhinisha sera mbaya''. Hatua hiyo inaendeleza kuwatoza kodi muhimu matajiri huku ikiwaondolea mzigo watoaji huduma za bima ili kuweza kuwapunguzia malipo watu masikini wanaohitaji huduma ya afya. M...